Soko la nguo mtandaoni kwa Tanzania. Maduka yanauza nguo zao, wateja wanalipa kwa simu, na kila kitu kipo kwa Kiswahili na Kiingereza.
Maelezo kamili ya mradi huu
PambaKali inaleta maduka ya nguo ya Tanzania pamoja kwenye soko moja la mtandaoni. Mteja anaangalia maduka na makundi, anachuja kwa bei au ofa, kisha anachagua saizi na rangi. Analipa kwa simu kupitia PigaPay na anafuatilia kila oda kwa SMS mpaka imfikie.
Kila duka lina dashboard yake. Muuzaji anaweka bidhaa na stock ya kila saizi, anaweka discount codes na Ofa Kali za muda mfupi zenye saa ya kuhesabu, anajibu maswali ya wateja, anasimamia oda na kufuatilia mapato na malipo yake. Timu ya PambaKali inakubali maduka mapya na kusimamia malipo, payouts, refunds, reviews na settings kwenye admin panel.
PambaKali pia ina vitu vilivyotengenezwa kwa jinsi watu wa hapa wanavyonunua nguo. Kwa Sare, mtu mmoja anaanzisha oda ya kikundi kwa harusi au send-off na kutuma link, na kila mgeni anachagua saizi yake na kulipa sehemu yake. Kwa Nijulishe, mteja anapata SMS moja saizi iliyoisha ikirudi, au bidhaa ya wishlist yake ikishuka bei.
Imetengenezwa kwa simu kwanza, na unaweza kuiweka kwenye simu kama app.
Tulichokabiliana nacho
Jinsi Tulivyozitatua
2026
PigaTech SoftCompany
Completed
Matokeo