New Completed

PigaPOS

Business Management PigaTech SoftCompany 2026

Mfumo wa mauzo (POS) uliotengenezwa Tanzania kwa maduka, kantini, migahawa, saluni na huduma nyingine: uza haraka, fuatilia stoo, wateja na madeni, toa risiti kwa WhatsApp, pokea malipo kwa simu na uuze hata bila intaneti.

Muhtasari wa Mradi

Maelezo kamili ya mradi huu

PigaPOS inaendesha siku nzima ya biashara kutoka kwenye simu, tableti au kompyuta. Kaunta inauza kwa kugusa au kwa barcode na inaendelea kufanya kazi bila intaneti hadi siku 7, kisha inatuma mauzo intaneti ikirudi. Mmiliki anaona stoo, manunuzi na wasambazaji, wateja, madeni na akaunti za kulipia kabla, hesabu za kila zamu, ripoti na matawi yote sehemu moja. Kila aina ya biashara ina vyake: kantini zinapata ubao wa oda za jikoni, skrini ya oda kwa wateja na menyu kwenye TV; migahawa inapata meza, wahudumu, tiketi za jikoni, kugawa bili na oda kwa QR code kutoka mezani au chumbani hotelini; saluni na huduma nyingine zinapata miadi kwa kila mfanyakazi, ukumbusho kwa SMS na kamisheni. Wateja wanapata risiti kwa WhatsApp au SMS, wanatoa maoni, wanalipa kwa simu kupitia PigaPay na wanauliza bei au salio lao kwa msaidizi wa WhatsApp. Kila biashara inaweza kufungua duka la mtandaoni bure. Mmiliki anapata tahadhari za wizi, ofa na happy hour, orodha ya Nunua Tena kwa wasambazaji na ripoti ya jioni. Kila kitu kiko kwa Kiswahili na Kiingereza, na risiti zinaweza kutumwa TRA kupitia mfumo wa VFD.

Changamoto

Tulichokabiliana nacho

  • 1. Biashara ndogo bado zinaandika mauzo na madeni kwenye daftari, hivyo stoo inapotea na madeni yanasahaulika
  • 2. Intaneti na umeme vinakatika, na mifumo mingi ya POS inaacha kuuza wakati huo
  • 3. Wamiliki hawawezi kukaa dukani siku nzima na hawajui pesa, stoo au punguzo vikienda vibaya
  • 4. Wateja wanataka kulipa kwa simu na kupata risiti, lakini kuhakiki malipo kwa mkono ni polepole na rahisi kudanganya
  • 5. Mifumo mingi ya POS iko kwa Kiingereza tu na imetengenezwa kwa aina moja ya biashara

Suluhisho

Jinsi Tulivyozitatua

  • 1. Kaunta inayouza bila intaneti hadi siku 7 na kutuma mauzo yenyewe intaneti ikirudi
  • 2. Stoo, madeni, akaunti za kulipia kabla na hesabu za kila zamu, pamoja na ukumbusho wa madeni kwa SMS
  • 3. Tahadhari za wizi kwa mmiliki (mauzo yaliyofutwa, upungufu wa pesa, vitu vilivyoondolewa, kubadilisha bei) na ripoti ya jioni kwa SMS na barua pepe
  • 4. Malipo kwa simu kupitia PigaPay, yanayorekodiwa tu baada ya malipo kuthibitishwa
  • 5. Zana kwa kila biashara: ubao wa jikoni na menyu kwenye TV, meza na oda kwa QR code, miadi na ukumbusho kwa SMS
  • 6. Kiswahili kwanza, na Kiingereza kwa kugusa mara moja
Teknolojia Zilizotumika
PHP 8.2 MariaDB / MySQL JavaScript (ES6+) HTML5 and CSS3 Progressive Web App (works offline) Web Push notifications PigaPay mobile money API WhatsApp Cloud API Mambo SMS API PHPMailer (email) TRA VFD API QR codes and barcode scanning Editor.js Font Awesome Automated browser tests (Chrome DevTools Protocol)

Mwaka wa Kukamilika

2026

Mteja

PigaTech SoftCompany

Hali

Completed

Matokeo na Athari

Matokeo

  • Siku 7 za kuuza bila intaneti
  • Aina 6 za biashara kwenye mfumo mmoja
  • Mitandao 4 ya pesa kwa simu kupitia PigaPay
  • Lugha 2, Kiswahili kwanza
  • Wamiliki wanaona dalili za wizi siku hiyo hiyo
Ongea nasi WhatsApp

Mawasiliano

Tupigie Simu
+(255) 678 520 538
WhatsApp
+(255) 678 520 538
Barua Pepe
info@pigatechsoft.com

Msaidizi wa AI

Mtandaoni
Imenakiliwa!