Live Platform Completed

Agiza Chakula

Food & Delivery PigaTech SoftCompany 2026

Mfumo wa kuagiza chakula wa PigaTech SoftCompany kwa Tanzania. Mteja anaagiza kutoka kwa wauzaji wa karibu, analipa kwa simu au cash, na anafuatilia oda yake kwenye ramani. Muuzaji anasimamia menyu, oda, saa za kazi na mauzo kwenye app moja.

Muhtasari wa Mradi

Maelezo kamili ya mradi huu

Agiza Chakula imetengenezwa na inaendeshwa na PigaTech SoftCompany. Inawaleta mtandaoni wauzaji wadogo wa chakula wa Tanzania (mama/baba lishe, kantini na migahawa midogo) bila kila mmoja kuhitaji tovuti au app yake, na inampa mteja sehemu moja ya kuaminika ya kupata chakula karibu naye.

Mteja anaona wauzaji wa karibu yake pamoja na menyu, picha, bei na saa zao za leo, na anaagiza kwa kubonyeza mara chache: analetewa kwa boda, bajaji au gari, au anachukua mwenyewe. Analipa kwa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money (kupitia PigaPay) au cash. Anafuatilia oda kwenye ramani yenye njia halisi na dakika zilizobaki, na anaipokea kwa code yake ya siri.

Mteja akilipa kwa simu, Agiza Chakula inaitunza pesa salama na kumpa muuzaji baada ya chakula kufika tu. Mteja anabonyeza "Nimepokea" au "Sijapokea", na admin anaamua kama kuna tatizo.

Muuzaji anapata duka kamili: ukurasa wa menyu yake na QR code, oda mpya zenye mlio, vyakula maalum vya leo, ada zake za usafiri, njia za malipo (cash, simu au vyote), saa za kazi za kila siku zinazofungua na kufunga duka lenyewe, na muhtasari wa mauzo.

Mfumo mmoja wa PHP unahudumia tovuti na API ya JSON ya app za Flutter zilizopo Google Play, Microsoft Store, Snap Store na apt yetu wenyewe kwa Kali, Debian na Ubuntu. Kiswahili kwanza, na Kiingereza kamili.

Changamoto

Tulichokabiliana nacho

  • 1. Kuonyesha njia halisi ya kuleta chakula na muda wa kufika bila kulipia huduma za ramani
  • 2. Kupunguza gharama za SMS huku watu wakijulishwa kila hatua
  • 3. Watumiaji wengi wanapenda Kiswahili, lakini mfumo lazima ufanye kazi pia kwa Kiingereza
  • 4. Kuhakikisha oda sahihi inamfikia mteja sahihi
  • 5. Kulinda pesa ya mteja anapolipa kabla chakula hakijafika
  • 6. Wauzaji kusahau kufungua au kufunga duka lao
  • 7. Mfumo mmoja kwa simu, kompyuta za kaunta na tovuti

Suluhisho

Jinsi Tulivyozitatua

  • 1. OpenStreetMap na OSRM: njia na dakika zinabadilika muuzaji anaposogea
  • 2. Taarifa za app kwanza, SMS fupi pale tu inapohitajika
  • 3. Kiswahili kwanza, na Kiingereza kamili kwenye tovuti, app na Google
  • 4. Code ya siri ambayo mteja anampa muuzaji anapoletewa
  • 5. Agiza Chakula inatunza pesa mpaka mteja abonyeze "Nimepokea", au admin aamue
  • 6. Saa za kazi za kila siku: duka linafunguka na kufunga lenyewe
  • 7. App moja ya Flutter kwa Android, Windows na Linux, kwenye API moja na tovuti
Teknolojia Zilizotumika
PHP 8 MySQL / MariaDB JavaScript Bootstrap 5 Flutter (Android, Windows, Linux) Leaflet and OpenStreetMap OSRM road routing Firebase Cloud Messaging PigaPay (mobile money) Google Sign-In SMS gateway Snap and apt packages (Linux) Schema.org and hreflang SEO

Mwaka wa Kukamilika

2026

Mteja

PigaTech SoftCompany

Hali

Completed

Matokeo na Athari

Matokeo

4mifumo: tovuti, Android, Windows na Linux
3mitandao ya pesa kwa simu, pamoja na cash
2lugha: Kiswahili na Kiingereza
  • Wauzaji wadogo wa chakula wanapata menyu yao mtandaoni, QR code na mfumo wa oda
  • Pesa ya mteja inamfikia muuzaji baada ya chakula kufika tu
Ongea nasi WhatsApp

Mawasiliano

Tupigie Simu
+(255) 678 520 538
WhatsApp
+(255) 678 520 538
Barua Pepe
info@pigatechsoft.com

Msaidizi wa AI

Mtandaoni
Imenakiliwa!