Zana 50+ za bure kwa wabunifu mahali pamoja - badilisha video, audio, picha na PDF, ondoa background ya picha, tengeneza subtitles, lyric video, meme na sticker. Zana nyingi zinafanya kazi kwenye browser yako, kwa hiyo mafaili yako hayatoki kwenye simu au kompyuta yako.
Maelezo kamili ya mradi huu
PigaTools ni website ya zana kwa wabunifu, wanafunzi na biashara ndogo Tanzania na kwingineko. Inaleta zana 50+ za kila siku mahali pamoja, kwa Kiingereza na Kiswahili - converter ya video na audio, kubadilisha ukubwa na kukata picha, kuondoa background ya picha kwa AI, zana za PDF, kusoma maandishi kwenye picha (OCR), kutengeneza QR code, rangi (palette), meme na sticker, maandishi kuwa sauti, subtitles kwa AI, lyric video na video za WhatsApp status.
Kazi nzito inafanyika kwenye browser ya mtumiaji kwa WebAssembly na AI, kwa hiyo ni ya haraka, mafaili yanabaki salama na inafanya kazi kwenye hosting ya bei nafuu. Zana nyingi ni bure. Pro (kuanzia TSh 3,000 kwa wiki) inaondoa vikomo vya kila siku na kufungua ubora wa juu zaidi. Wateja wanalipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa kupitia PigaPay, na Pro inawashwa yenyewe. Pia ina Studio ya kuhifadhi kazi, mipango ya timu, maelekezo ya jinsi ya kutumia, app ya kuweka kwenye simu, na ku-share mafaili kwenda PigaTools moja kwa moja kutoka app nyingine.
Tulichokabiliana nacho
Jinsi Tulivyozitatua
2026
PigaTech SoftCompany
Completed
Matokeo
# Products page